KESI YA JUMUIYA DMV

Kesi iliyokuwa imefunguliwa kupinga uchaguzi wa Jumuiya ya DMV ilisikilizwa jana na juzi katika mahakama ya Montgomery County. Kesi Hiyo ilifunguliwa na Bwana Liberatus Mwangombe, Solomon Cris, Ruth Mukami na Baybe Mgaza kupinga uchaguzi wa jumuiya. Pia katika kesi hiyo kulikuwa na tuhuma mbalimbali za ubadhilifu.

Mahakama imetupilia mbali madai yote na kuwapa ushindi Washitakiwa. Kutokana a uamuzi huo, uchaguzi wa DMV ulikuwa halali na hakukuwa na ubadhilifu wowote. Repoti kamili kutoka mahakamani itatumwa na kusambazwa mara itakapo kuwa Tayari.

No comments:

Post a Comment