Stori: MAYASA MARIWATA NA HAMIDA HASSAN
MUUZA nyago anayefanya poa Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ anadaiwa kumkimbia mama yake aliyekuwa akiishi naye maeneo ya Kinondoni na kwenda kuishi na mwanaume (jina linahifadhiwa kwa sasa) maeneo ya Tabata jijini Dar.
Chanzo makini kimetutonya kuwa, tangu mwanadada huyo awe staa, amekuwa si mtu wa kukaa na mama yake badala yake amekuwa kiruka njia, usiku anaenda klabu, mara kasafiri kwenda nje lakini siku zote analala na kuamkia kwa mwanaume huyo.
“Unajua Kidoa siku hizi kamkimbia kabisa mama yake, muda mwingi yupo kule Tabata kwa bwana wake wakati bi mkubwa alishazoea kuishi naye,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzipata nyeti hizo, Ijumaa lilimtafuta Kidoa ambapo alikiri kuwepo Tabata kwa ‘mtu’ wake akieleza kuwa, bi mkubwa huwa anakwenda kumuona mara mojamoja.
No comments:
Post a Comment