Sakina Kisukari na njemba aliyekutwa naye gesti.
Stori: Francis Godwin, UWAZI
IRINGA: Mke wa kigogo mmoja wa serikali Mkoa wa Morogoro ambaye ni mwenyeji wa Wilaya ya Iringa, Kijiji cha Mlangali, Sakina Kisukari, amenaswa akiwa katika nyumba ya kulala wageni (gesti) akiwa na mfanyabiashara ambaye inadaiwa ni mchepuko wake.
Tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo eneo la Mshindo, Iringa baada ya kufyatuka mtego uliowekwa na mume wa mwanamke huyo kwa kushirikiana na gazeti hili kabla ya kuwashirikisha polisi ili kuepusha damu kumwagika.
Walivyokutwa gesti.
Mtego huo uliwekwa kwa zaidi ya wiki mbili ili kufuatilia nyendo za mwanamke huyo ambaye aliondoka mkoani Morogoro anakoishi na familia yake kikazi na kuelekea Iringa kwa madai ya kwenda kuwasalimia ndugu zake.
Hata hivyo, baada ya bosi huyo wa serikali (jina lake limehifadhiwa kwa heshima ya kazi yake) kujaribu kupeleleza ili kujua kama kweli mkewe huyo yupo nyumbani kwa wazazi au kwa ndugu zake Iringa, aligundua hakuwepo hivyo kuanza msako wa kimyakimya kabla ya kutoa taarifa polisi kuhusu kupotelewa na mke.
Njemba akikodoa jicho.
Katika upelelezi wake, aligundua kuwa mke wake yupo na mchepuko katika nyumba ya kulala wageni ambayo mfanyabiashara huyo alikuwa amepanga kwa zaidi ya wiki mbili sasa akiwa na mkewe ndipo alipokwenda kumfumania akiwa chumbani.
Akisimulia mkasa mzima, kigogo huyo alisema kuwa alilazimika kufika mjini Iringa baada ya watu ambao aliwapa kazi ya kumsaka mkewe kurejesha taarifa Ijumaa jioni kuwa mkewe huyo alikuwepo katika nyumba hiyo ya kulala wageni.
“Nilifunga safari usiku na kuingia Iringa mjini saa 8 usiku, kabla ya kwenda eneo la tukio, nimekuja na cheti changu cha ndoa (nakala tunayo) tuliyofunga mwaka 2003 kama ushahidi wa ndoa yetu na nyumbani nimeacha watoto wetu watatu,” alisema.

Gazeti hili pamoja na polisi lilishuhudia kigogo huyo akimfumania mkewe baada ya kuomba wanausalama kushuhudia ili kuepusha machafuko kati ya mwenye mke na mgoni huyo ambaye alilipongeza jeshi la polisi kwa kufika kwani alisema uhai wake ungekuwa mashakani.
Akizungumza eneo la tukio akiwa chumbani, aliyefumaniwa aliyejitaja kwa jina mmoja la Hemed, alisema: “Ni kweli nimekuwa na mwanamke huyu kwa wiki mbili katika nyumba hii ya kulala wageni lakini alinidanganya kuwa hajaolewa ila ana watoto.”
Naye mwanamke huyo baada ya kuona watu wakiwa na mumewe, awali alimkana mume wake na kueleza kuwa ni shemeji yake lakini alipobanwa alikiri kuwa ni mumewe.

“Mimi kweli huyo ni mume wangu wa ndoa nilikuwa najitetea ili asinipige lakini naomba kusamehewa, ni shetani tu amenipitia kuchepuka,” alisema mwanamke huyo huku akifuta machozi.
Mumewe alimtaka mkewe amrudishie pesa zake zaidi ya Sh. milioni mbili pamoja na kitambulisho cha kazi na simu aliyoondoka nayo ili amwache aendelee na mfanyabiashara huyo.
Mumewe alimtaka mkewe amrudishie pesa zake zaidi ya Sh. milioni mbili pamoja na kitambulisho cha kazi na simu aliyoondoka nayo ili amwache aendelee na mfanyabiashara huyo.
No comments:
Post a Comment