Mabalozi wa Tanzania wakwama ughaibuni.

Uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli wa kuwarejesha nyumbani mabalozi waliomaliza muda wa utumishi wao umekwamishwa na ukata, imeelezwa.

Januari 25, mwaka huu, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alitangaza agizo la rais kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, kuwarejesha nyumbani mara moja mabalozi wawili ambao mikataba yao imekwisha.

Mabalozi hao ni Dk. Batilda Buriani aliyeko Tokyo Japan na Dk. James Msekela, aliyeko Rome, Italia.

No comments:

Post a Comment