Nay, Dayna Aibu Yao!

nay (1)Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa katika pozi la nusu utupu na msanii wa Bongo Fleva, Aisha Nyange ‘Dayna’.
NA BONIPHACE NGUMIJE, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Hii ni aibu yao! Picha zinazomuonesha staa wa Hip Hop anayetamba na ngoma ya Shika Adabu Yako, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa katika pozi la nusu utupu na msanii wa Bongo Fleva, Aisha Nyange ‘Dayna’ zimevuja pasipo wenyewe kujua.
nay (2)Katika baadhi ya picha hizo, Nay anaonekana akiwa amemkumbatia Dyna huku wakiwa hawana nguo za juu, yaani Nay hana vesti wala tisheti na hata Dyna akiwa hana nguo yoyote ya kumstiri juu.
Baada ya kuzidaka picha hizo gazeti hili lilivuta waya na kuwatafuta wahusika ambapo baada ya kumpata Nay na kumdadisi kama anabanjuka kimalovee na mwanadada huyo alikuwa na haya ya kusema;
nay (3)“Dah, hapana bwana, hizo picha hatukupanga zitoke. Kuna ambazo zilipitiliza si unajua wakati wa kupiga studio zipo ambazo huwa hamzitumii sasa sijui nani alizivujisha hizo mbaya.”
Baada ya kumalizana na Nay, Dyna naye alitafutwa ili kuifungukia ishu hii, ambapo baada ya kupatikana alidai zilikuwa ni picha za kwenye kava la ngoma yake ya Nitulize aliyomshirikisha Nay lakini alipoulizwa kuhusu zile zilizovuka maadili, alijibu:
“Aah! Hilo ni suala binafsi, lakini naomba iishie kufahamika kuwa Nay ni mtu wangu wa karibu lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, ilikuwa ishu ya kazi tu.”

No comments:

Post a Comment