Gari likitoka katika jengo hilo.
Stori: Amran Kaima, Ijumaa:
OpAresheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers hivi karibuni ilitumbua jipu la usalama katika jengo la Mlimani City baada ya kubaini uzembe f’lani kwenye geti la kutokea magari.
Ijumaa iliyopita ya Machi 18, 2016, mida ya kati ya saa 6:00 na 7:00 mchana, paparazi wetu alikuwa katika mizunguko yake, alipokatiza kwenye Barabara ya Survey kuelekea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliona mlingoti unaozuia na kuruhusu magari kutoka na kuingia ukiwa umeinuka huku kukiwa hakuna mtu yeyote.

Baada ya kubaini jipu hilo, paparazi aligeuza gari na kwenda kuingia kwenye jengo hilo kupitia geti lililopo upande wa Barabara ya Samu Nujoma ambapo alibonyeza kitufe kwenye mashine eneo la geti, ikatoka kadi na gari ikaingia.
Baada ya kuingia ndani, OFM haikukaa sana, ikaenda kwenye mashine iliyopo ndani ya jengo hilo, akaingiza kadi kisha akaruhusiwa kutoka bila kulipia.

Likiingia katika barabara kuu.
Eneo la geti la kutokea
Baada ya muda, paparazi alifika kwenye lile geti lililokuwa na tatizo nako kulikuwa vilevile, kwamba mlingoti ulikuwa umenyanyuka na hakukuwa na wale vijana wanaopokea kadi kama kuna tatizo kwenye mashine au kutoa msaada pale inapobidi.
Kufuatia hali hiyo, paparazi aliangaza macho huku na kule akashuka na kujaribu kutafuta kama angeona mtu wa kumpa kadi hiyo lakini hakuwepo ndipo akatoka nayo.

Kwa nini ni tatizo kutoka na kadi ile?
Kwanza, kwa nyuma imeandikwa kuwa ukiipoteza unatakiwa kulipa takriban shilingi 21,000 hivyo kwa mazingira hayo tayari Kampuni ya Chui System Ltd inayotoa huduma hiyo imepata hasara.
Pili, kwa kuwa ukiwa unatoka bila kuwa na kadi hiyo huwezi kuruhusiwa, kuna uwezekano baadhi ya magari yaliyotoka wakati mlingoti umeinuka hayakuwa na vigezo vya kuruhusiwa kutoka.

Uongozi unasemaje?
Kufuatia tatizo hilo, mwandishi wetu alimtafuta Meneja wa Kampuni ya Chui System, Solomoni Anampiu, alipopatikana alisema:
“Kwa kweli hilo ni tatizo, hairuhusiwi mtu yeyote kutoka na kadi hizo kwa kuwa tumetengeneza kwa gharama kubwa. Nakuomba popote ulipo nikutumie mtu aje aichukue.

“Huenda kulikuwa na tatizo lakini pia palistahili kuwepo mtu wa kupokea kadi hizo, wataandika ripoti ya kilichotokea.”
Baada ya muda, mtu aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Kampuni ya Chui System Ltd aliyepo Mlimani City, aitwaye Thabiti Fikirini alimpigia mwandishi simu akidai ameagizwa na bosi wake (Bwana Solomoni) amfuate popote alipo ili kuichukua kadi hiyo.
Hata hivyo, paparazi huyo alimtaka Thabiti kumuunganisha kwanza na watu wa usalama ili kujua kilichotokea lakini ushirikiano ulikuwa hafifu na mpaka tunakwenda mtamboni, kadi hiyo iko mikono mwa OFM akijipanga namna ya kuirudisha kwa wahusika.

No comments:
Post a Comment