Gigy Money alewa tilalila, azimika

IMG_2498Video Queen na Mtangazaji wa Runinga, Gifty Stanford ‘Gigy Money’ akiwa amezima baada ya kupiga mitungi.
HAMIDA HASSAN NA MAYASA MALIWATA
V ideo Queen na Mtangazaji wa Runinga, Gifty Stanford ‘Gigy Money’ juzikati alifakamia pombe kali na kujikuta akilewa tilalila hadi kuzimika ndani ya klabu moja iliyopo kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar.
inti huyo asiyeishiwa na vituko alinaswa na mapaparazi wetu akiwa kwenye hali hiyo Jumatatu liyopita (Jumatatu ya Pasaka) ambapo awali alionekana akinywa pombe kali huku akivuta sigara. Baada ya kupombeka kwa muda mrefu huku akionekana kama aliyekuwa na mawazo mengi, taratibu mdada huyo aliyejaaliwa shepu alianza kupoteza ‘netiweki’.
IMG_2491…Alianza mdogomdogo.
Haikuchukua muda refu akawa amezimika na kuwaacha watu waliokuwa wakimuangalia wakimjadili kwa namna ambavyo alikuwa hajitambui. “Huyu bwana pombe zitamuua, mwenyewe huwa anasema anakunywa kidogo tu, sasa mbona leo hadi kazima, asipoangalia wahuni watamfanyizia,” alisema kijana mmoja aliyekuwa eneo la tukio.
Baada ya muda mfupi, alifika dada mmoja aliyeonekana kujuana na Gigy (inaonekana alipigiwa simu) ambapo alimchukua kwa kumkokota kisha akampakiza kwenye Bajaj wakaondoka.
Siku moja baada ya tukio hilo, Ijumaa lilimpigia simu Gigy Money na kumuuliza kulikoni amekuwa na tabia ya kulewa hadi kuzimika alipopatikana alijibu: “Ni maisha yangu, haina haja kunifuatilia.”

No comments:

Post a Comment