Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika jiji la Houston, Texas na miji mingine ya jirani jana jioni (Jumamosi tarehe 24/04/2016) katika ukumbi wa Sienna ulioko mitaa ya Bissonet ilifanya Harambee iliyovunja rekodi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuurudisha mwili wa ndugu ya kipenzi Andrew Nicky Sanga aka Drew. Katika Harambee hiyo jumla ya $52,511 zilikusanywa kutokana na fedha taslimu na minada ya vitu mbalimbali vilivyotolewa na wanajumuiya na marafiki wa Drew kutoka mataifa mbalimbali. Ama kweli Andrew aligusa mioyo ya watu wengi sana katika safari yake hapa duniani. Kamera yetu ilikuwepo ukumbini kukuletea picha za tukio hilo .
| Marehemu Andrew Sanga enzi za uhai wake |
| Mchungaji akifungua Harambee kwa sala |
| Wanajumuiya wa Houston |
| Emmy akiwa na Dada wa marehemu |
| Zoe (binti wa marehemu Drew) akiwa ameshikilia picha ya baba yake |
| Wakina dada wa Drew wakiwa na Zoe na mama yake |
| Emmy, Zoe na shangazi wa Marehemu Andrew |
| Julius Shayo wa North Carolina ( rafiki wa karibu wa Drew aliyempokea alipofika USA) |
No comments:
Post a Comment