MAGUFULI AONDOA KIGOGO MWINGINE ILUKLU

Kwa mujibu wa mabadiliko yaliyotangazwa na Ikulu jana, Rais Magufuli amemwondoa Ikulu Gelasius Byakanwa, ambaye alikuwa msaidizi wake wa karibu.

Taarifa ya iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ilisema mpaka mabadiliko hayo yanafanyika jana, Byakanwa alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi.

Taarifa hiyo iliyomnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi ilisema Rais Magufuli amempeleka kigogo huyo kuwa Mkuu wa Wilaya Hai mkoa wa Kilimanjaro, kuchukua nafasi ya Antony Mtaka.

Katika uteuzi mpya wa wakuu wa mikoa hivi karibuni, Mataka aliteuliwa na Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Kigogo huyo wa Ikulu anakuwa wa pili kuondolewa Ikulu baada ya Sefue aliyeondolewa katika mabadiliko yaliyotangazwa Machi 7.

No comments:

Post a Comment