Mwanafunzi Armo Halwan akimuelekeza Rais wa Marekani,Barack Obama anavyoweza kutumia simu kuendesha cha kufanyia usafi ( Vacuum Cleaner) kilichobuniwa na wanafunzi wa Baruch Collage Campus High School ya Jijini New York kupitia timu yao ya ufumbuzi (Invent Teams)katikati ni Wendy Ni na anayefuatia ni Stephen Mwingira ( mtanzania) anaonyesha namna gani kifaa hicho kinavyofanya usafi kwenye njia za treni za ardhini ( Subways).
Stephen Mwingira na Wendy Ni, wakiangalia kwa makini jinsi Rais Obama anavyoelekezwa namna ya kutumia simu kuendesha mashine hiyo katika Onyesho la ubunifu wa kisayansi ambalo lilifadhiliwa na Rais Barack Obama katika Ikulu ya Rais ( White House Science Fair 2016)
Oh "Kumbe kinafanya kazi hivi" ndivyo anavyoelekea kusema Rais Obama mara baada ya kuweza kukiendesha kifaa hicho kwa kutumia simu, aliyechuchuma ni Stephen Mwingira ambaye pamoja na Wendy Ni na Armon Halwan walipata fursa ya kuonyesha ubunifu wao katika onyesho la mwisho lililoandaliwa na Rais Barack Obana na kufanyika White House April 13. 2016
April 13, 2016, Rais wa Marekani, Barack Obama, alifadhili onyesho la mwisho katika utawala wake, onyesho lililohusu ubunifu katika Nyanja za sayansi ambalo limewahusisha wanafunzi kuanzia shule za awali,msingi hadi za sekondari kutoka States mbalimbali za Marekani.
Kwa miaka sita tangu mwaka 2010, Kiongozi huyo wa Marekani amekuwa akifadhili onyesho hilo lijulikanalo kama White House Science Fair ambalo limekuwa likifanyia katika Ikulu yake (White House) lengo likiwa ni kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi, hisabati ,teknolojia na ufundi ( STEM)na hivyo kuibua vipaji vya ubunifu mwiongoni mwa wanafunzi ( young inventors) .



No comments:
Post a Comment