Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametaja mshahara wake kuwa ni Tsh mil 9.5, huku akiahidi atatoa Salary slip zake punde akitoka mapumzikoni Chato.
Hiyo imetokea wakati wa kipindi cha magazeti leo tarehe 01/04/2016 ambapo watangazaji walisoma habari iliyoandikwa na gazeti la nipashe kuwa Zitto na Lissu waomba ataje Mshahara wake na ukatwe kodi.
Wakiwa katika mjadala huo, walipokea taarifa kuwa Rais kawasikia na katuma taarifa ofisi za Clouds kujuza mshahara wake kuwa ni mil 9.5 na atatoa stakabadhi zake akirudi Dar.
Huo ndio mshahara alioukuta na hata Rais Kikwete alikuwa akilipwa kiasi hicho pia.
Chanzo: Clouds 360
No comments:
Post a Comment