Davina: Hata niachike mara 100, napigania haki

davinaStori: Imelda Mtema, Wikienda
Dar es Salaam: Mwigizaji wa kitambo Bongo, Halima Yahaya ‘Davina’  amefunguka kuwa, hata watu wakisema kila mara anaolewa na kuachika yeye hatajali maneno yao kwa vile hata anapokuwa kwenye ndoa hakubali haki yake kudidimizwa.
Davina aliliambia Wikienda kuwa ni rahisi kwa watu kusema anaachika hovyo bila kujua sababu zinazofanya mtu kuondoka kwenye ndoa.
“Acha watu waseme naachika hovyo kwani hata kama nikiachika mara 100, sijali kwani kikubwa ni kupata haki yangu ya msingi kama mwanamke,” alisema Davina anayedaiwa kuachika kwenye ndoa yake.

No comments:

Post a Comment