MABASI YA HARAKA YAANZA KWA KISHINDO

Dereva wa basi la mwendo kasi akitoa maelekezo kwa abiria mara baada ya usafiri huo kuanza kwa kishindo jana.
KAMPUNI ya UDA-RT jana imeanza rasmi kutoa huduma ya mabasi yaendayo haraka katika Jiji la Dar es Salaam kwa kutumia mabasi 39 huku kukiwa na mwitikio mkubwa wa wananchi waliojikuta wakifanya utalii wa ndani kwa kuzunguka na mabasi hayo jambo lililoleta adha kwa watumiaji wengine.

Huduma hiyo ilianza jana kati ya saa tano asubuhi na kubeba abiria bila kulipia, kabla ya kuanza kulipa kuanzia kesho kwa nauli ya kati ya Sh 650 na 800 kwa safari moja. Usafiri huo ulianza jana na kwa mabasi machache na kwa siku mbili wananchi hawatalipa nauli na kazi inayofanyika ni kutoa elimu kwa wananchi wakiwa ndani ya mabasi ya namna ya kutumia mabasi hayo.

No comments:

Post a Comment