MAGUFULI: HAPA MKONG'OTO TU

Rais Dk John Magufuli.
RAIS John Magufuli amesisitiza kwamba kamwe hatakubaliana na wafanyabiashara wachache wanaotaka kuwaumiza Watanzania na kuitakia mabaya nchi, na atawashughulikia bila kujali vyama vyao.

Alisema kuna kikundi cha wafanyabiashara wachache sana kila kitu wanataka wafanye wao bila hata kuwahurumia Watanzania na wanataka kuiendesha nchi wanavyotaka ikiwa ni pamoja na kuingiza bidhaa wakati wowote wanavyotaka na kuwaumiza Watanzania, hilo halitakubalika kamwe.

“Hapa kwangu ni mkong’oto tu. Kwa wale wafanyabiashara wenye kuitakia mabaya nchi hilo halitavumiliwa… awe CCM, CHADEMA au CUF atashughulikiwa kikamilifu,” alisema Rais Magufuli jana mjini hapa kabla ya kuzindua rasmi jengo la PPF la ghorofa 11 na jengo la Mfuko wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) lenye urefu wa ghorofa 13, mbili za chini yote yakiwa na gharama ya zaidi ya Sh bilioni 60.

No comments:

Post a Comment