Kutoka kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania, John Magufuli, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kupitia mtandao wa twitter ameweka namba maalum ambazo zitakuwa hewani kila siku kwa saa 24 kwa ajili ya kupokea taarifa zozote kutoka kwa raia wema zinazohusu uharifu, ajali, moto na nyingine ambapo baada ya kupokea taarifa hizo eshi la Polisi litazifanyia kazi mara moja.
Kupiga namba hizo ni bure ambapo mwananchi hatotozwa kiwango chochote cha pesa na anaruhusiwa kupiga kupitia mtandao wowote wa simu.
Alichokiandika Mwigulu kwenye twitter: “Piga simu namba 111 au 112 kutoa taarifa jeshi la polisi kuhusu uhalifu wowote,utapata msaada kwa haraka.”
#Piga simu namba 111 au 112 kutoa taarifa jeshi la polisi kuhusu uhalifu wowote,utapata msaada kwa haraka.







No comments:
Post a Comment