KATIKA hali ya kufurahisha unaweza kusema kuwa hii ni staili mpya na ya aina yake kuuza maembe na tawi lake katika Jiji la Dar baada ya kukuta muuzaji akifanya hivyo.
Tukio hilo limebambwa katika eneo la Tabata Magengeni jijini Dar es Salaam ambapo mtandao huu ulimkuta muuzaji aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhan Rashid akiuza maembe kwa staili hiyo na tawi lake.
Baada ya kupata nafasi ya kumhoji muuzaji huyo sababu ya kuuza maembe pamoja na tawi lake alisema kuwa lengo lake kubwa ni kuvutia wateja kwani wengi wanapenda maembe ambayo hayajavundikwa hivyo na kumpelekea yeye kupata wateja wengi kwa staili hiyo.
“Ujue mimi mwenyewe ndiye ninayeotesha miti ya miembe na kuipanda kwenye shamba langu hivyo sioni sababu ya kuuza na tawi lake na hii imenifanya niuze matunda safi yanayopendwa na wengi pia ninauza miche ya miembe kwa yeyote anayeihitaji anaweza kunipigia simu kwa namba +255 0623060769 na mteja wangu ataweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo ya matunda,” alijifagilia muuzaji huyo.
Katika hatua nyingine staili kama hiyo ya kuuza maembe na tawi lake imekuwa ikionekana katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kama vile Kariakoo, Kitunda, Charambe na maeneo mengine ambayo hupelekea wauzaji kuonekana wakipata wateja wengi.
NA DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment