Watu saba wamefariki dunia kwenye kijiji cha Chemba, mkoani Dodoma na wengine zaidi ya 14 wamelazwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo kutokana na kukumbwa na ugonjwa usiofahamika.
Ugonjwa huo umekuja baada ya watu hao kula nyama ya ng’ombe aliyechinjwa na kugaiwa kwa baadhi ya watu kwenye kijiji hiko. Mmoja wa mzee wa familia iliyokumbwa na ugonjwa huo amesema, “Tulikula nyama tuliyopewa na jirani yetu na jioni tukala ugali na maziwa. Tulianza kuugua na baada ya siku tatu kutapika na kuharisha.”
Dalili za ugonjwa huo ni kutapika,kuharisha,kupata rangi ya manjano machoni na sehemu zingine na tumbo kuvimba na kujaa maji. Lakini pia ugonjwa huo umeuwa paka pamoja na mbwa ambao walikula nyama hiyo.
No comments:
Post a Comment