Dar es Salaam. ongezeko la abiria hasa wanafunzi limesababisha upungufu wa mabasi yanayotoa huduma kutoka Dar es Salaam kwenda mikoani na kusababisha wasafiri wengi kukwama.
Abiria hao wameonekana wameketi chini kusubiri usafiri bila matumaini na wengine wakiwa katika foleni ndefu kwa ajili ya kukata tiketi ili kujihakikishia safari kesho.
Mmoja wa wakatisha tiketi, Shaffik Ally amesema tatizo la usafiri lipo zaidi kwa mabasi ya Morogoro, Moshi, Arusha na Iringa.
“Kwa mikoa ya mbali kama Mwanza, Mbeya, Kagera na Kahama ukitaka tiketi siku mbili kabla ya safari hakuna shida na unapata usafiri wa uhakika, lakini mikoa hii ya karibu ambayo watu walizoea hata kuja asubuhi na kupata usafiri, hali imekuwa tofauti kabisa,” amesema.
No comments:
Post a Comment