Ethiopia Yazima Mitandao Yote ya Kijamii


Access-Facebook-When-It-Is-Blocked
SERIKALI nchini Ethiopia imefunga mitandao yote ya kijamii ya mitandao ya Facebook, Twitter, Instagram na Viber baada ya kuvuja kwa mitihani ya mwisho ya kujiunga na elimu ya juu. Mitandao yote imefungwa hadi mitihani itakapomaliza siku ya Jumatano.
Hiyo imetokana na maswali ya mitihani hiyo kuchapishwa kwenye mitandao, hali iliyoleta mtafaruku mkubwa na kuichafua serikali ya Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn Boshe. Baada ya kuvuja kwa mitihani hiyo serikali iliahirisha zoezi zima la mitihani nchi nzima.
instagram-blocked-occupycental-hong-kong-20140929_136C87C0D9184BF3817C3714C434B832
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari msemaji wa serikali, Getachew Reda, alisema, “tumeifunga, ni zoezi la muda mfupi hadi siku ya Jumatano, mitandao ya kijamii imedhihirisha inawalemaza wanafunzi wetu.”
Ethiopia ni miongoni mwa nchi za kwanza barani Afrika kuwekeza katika matumizi ya intaneti, ilianza mwaka 2006. Wiki iliyopita Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kwamba kufunga intaneti ni uvunjaji wa haki za binadamu.
Wizara ya elimu ya nchi hiyo imesema jumla ya wanafunzi 254,000 wanakadiriwa kufanya mitihani yao ya mwisho.

No comments:

Post a Comment