Shilole sikio la kufa!

SHILOLE (1)Zuena Mohammed ‘Shilole’ akiwa stejini.
Hamida Hassan, Risasi Jumamosi
Mwanamuziki Zuena Mohammed ‘Shilole’ anaonekana ni sikio la kufa baada ya hivi karibuni kupanda tena stejini na kupafomu huku akiacha wazi sehemu zake ‘muhimu’.
shilole (1)Awali, msanii huyo alifanya kitendo kinachofanana na hicho Mei 9, mwaka 2015 ambapo alipokuwa kwenye onyesho la muziki nchini Ubelgiji ulicheza uchi hivyo Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) likampa adhabu ya kutojishughulisha na sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.
SHILOLE (2)Kufuatia adhabu hiyo, wadau wa muziki walitarajia mwanadada angebadilika lakini cha ajabu mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa anafanya shoo ndani ya Ukimbi wa Club Bilcanas alionekana akiwa amevaa kichupi na tisheti nyeupe.
Shuhuda wetu aliyefuatilia shoo hiyo mwanzo mwisho alisema kuwa, Shilole licha ya nguo ya kihasara aliyokuwa amevaa, kuna wakati alikuwa akiinama na kuacha ‘mzigo’ wake wazi huku nguo yake ya ndani nyeusi kimvuka kila mara.
SHILOLE (3)“Kwa kweli kile kinguo alichovaa Shilole kwenye ile shoo pale Bilz ni noma, si alionywa yule asifanye maonesho kwa kukiuka maadili, mmh! Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa,” alisema shuhuda huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Aidha, mdau mwingine wa muziki aliyeona video ya shoo hiyo mtandaoni ambaye naye aliomba asijulikane, alimtetea Shilole kwa kusema: “Sasa jamani kwenye shoo kama ile tena klabu, mlitaka avae kama anaenda kanisani au msikitini? Acheni ushamba bwana.”
SHILOLE (4)Mwandishi wetu alifanya jitihada za kutaka kuongea na Shilole juu ya shoo hiyo na jinsi alivyokuwa amevaa lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Gazeti hili linamshauri Shilole kujiamini na kufanya shoo za kistaarabu kwa kuwa muziki wake ni mtamu sana na amejaalia ustadi wa kukata mauno kiasi kwamba hata asipovaa nguo za kihasara, bado atadatisha tu.

No comments:

Post a Comment