Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe Ummy Mwalimu
Idadi ya watu waliofariki kutokana na kuugua ugonjwa wa ajabu ulioripotiwa mkoani Dodoma, imefikia 11.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema hayo jana katika taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari kupitia kurugenzi ya mawasiliano ya wizara hiyo.
Alisema kwamba, idadi ya walioripotiwa kuugua ugonjwa huo nayo imeongezeka na kufikia 43 hadi kufikia Julai 3, mwaka huu baada ya ugonjwa huo kuripotiwa Juni 13 mwaka huu.
“Ugonjwa huo uliripotiwa Juni 13, mwaka huu wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma na hadi kufikia jana (juzi), kulikuwa na wagonjwa 43 na vifo 11.
No comments:
Post a Comment