Hull, Uingereza
WATU zaidi ya 3200 wamekusanyika na kusherehekea utamaduni wao wakiwa kwenye huku wakiwa wamevua nguo zao zote (utupu) katika Mji wa Hull, Uingereza ikiwa ni tukio la kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni.
Katika tukio hilo lilitokea Jumamosi ambapo washiriki walijipaka miili yao rangi ya bluu-baharina kisha kupigwa picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull.
Mradi huo unatekelezwa na mpiga picha Spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya Sanaa ya Ferens Art Gallery.
Picha zilizopigwa siku ya tukio hilo, zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja.
Tunick, anayetoka New York, amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal, Mexico City na mjini Munich nchini Ujerumani Germany.
“Mavazi ni Sanaa ya mtu mwingine,” anasema.
“Fashoni ni Sanaa. Kwa kuondoa hilo (mavazi), nitakuwa nafanya kazi na usawa na maumbile katika umaridadi wake.”
Watu karibu 3200 walijiandikisha kupigwa picha tangu wazo hilo litangazwe mwezi Machi mwaka huu huku Baraza la Mji wa Hull likifunga baadhi ya barabara wakati wa shughuli hiyo Jumamosi asubuhi.






No comments:
Post a Comment