LICHA ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuwataka waendesha bodaboda (pikipiki) na abiria wao kutii sheria ya kuvaa kofia (helmet) na kutopakiza zaidi ya abiria mmoja (mshikaki), kamera yetu imewanasa baadhi ya abiria wakiwa wamepakizwa mshikaki pasipo kuzingatia agizo hilo la mkuu huyo.
Tukio hilo lilijiri katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi eneo la ‘Sayansi’ Kijitonyama, jijini Dar, ambapo abiria walikuwa hawajavaa helmet na walikubali kubebwa kwa mtindo wa mshikaki.
NA DENIS MTIMA/GPL

No comments:
Post a Comment