SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WAGANGA WAKUU WANAOWATOZA FEDHA ZA MATIBABU WAJAWAZITO, WAZEE NA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (kushoto ) akisisitiza jambo kuhusu umuhimu wa waganga Wakuu wa Hospitali za Umma kusimamia utekelezaji wa Sera na miongozo ya Afya katika  maeneo yao ya kazi.

Na Aron Msigwa - Dar es salaam. 

Serikali imesema kuwa haitamvumilia Mganga mkuu yeyote wa Hospitali ya Umma atakayebainika kuwatoza fedha wananchi walio katika kundi la watu wanaotakiwa kupata matibabu bure  wakiwemo wazee wasiojiweza, wajawazito na watoto  walio na umri chini ya miaka 5.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo jijini Dar es salaam kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya wananchi walio katika makundi hayo katika maeneo mbalimbali kudaiwa fedha katika hospitali hizo.


Serikali hatutamvumilia Mganga Mkuu yeyote wa hospitali ya umma anayetoza fedha kwa mwanamke mjamzito, kwa mtoto mwenye umri chini ya miaka 5 na mzee asiyejiweza, hatujabadilisha Sera " Amesisitiza Mhe.Ummy.

No comments:

Post a Comment