KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA KWA KOSA LA WIZI WA GARI
Mnamo tarehe 09.08.2016 saa 18:00hrs jioni huko Masasi Mjini kwenye gereji ya magari, Kikosi Maalum cha Kupambana na wizi wa Magari cha Polisi Kanda maalum cha Dar Es salaam kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa OMARY GILLIAD OMARY (35) kazi dereva kwa wizi wa gari. Mtuhumiwa alikamatwa kwa wizi wa gari No: T.612 AUJ aina ya Toyota Hiace mali ya mlalamikaji KAISARI MWALIMU YUSUFU (26) Mfanyabiashara mkazi wa Sinza.
Gari hilo iliyoibiwa tarehe 25.06.2016 likiwa limeegeshwa nyumbani kwa mlalamikaji maeneo ya Sinza ambapo mtuhumiwa alichukua gari hilo kwa nia ya kufanya kazi.
Baada ya mtuhumiwa kupewa gari hilo aliipeleka mafichoni Masasi Mjini mkoani Mtwara ambapo Kikosi cha Kupambana na Wizi wa Magari Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar Es salaam kilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa pamoja na kielelezo gari. Mtuhumiwa anahojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa mahakamani kujibu shutma inayomkabili dhidi yake.
KINARA MWIZI WA VIFAA VYA MAGARI AKAMATWA AKIWA NA VIFAA MBALIMBALI VYA MAGARI
Kikosi maalum cha kupambana na wizi wa magari cha Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa hatari anayejihusisha na wizi wa magari na viafaa vyake. Mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 01/08/2016 majira ya saa 08:30 usiku, maeneo ya amani mtaa wa kongo askari wakiwa doria walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aitwaye SALUMU S/O ISSA @HASSANI (43) Mkazi wa mbagala akiwa na (1).SIDE MIRROR 12 (2). SITE MIRROR 11(3) CAMP BAMPA 24 (3).PLATE SIDE MIRROR 44 (4) VITASA28 (5).SIDE LAMP 11 (6).INDICATOR 17 vifaa hivyo Vyote vikiwa ni mali za wizi akiwa ameviiba na baada ya kumhoji alikiri kuhusika na wizi huo. Mtuhumiwa huyo atapelekwa mahakamani wakati wowote upelelezi utakapokamilika.
TAARIFA YA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KANDA MAALUM YA D’SALAAM KUANZIA TAREHE 21.08.2016 HADI TAREHE 22.08.2016.
Taarifa ya Kikosi cha Usalama barabarani Kanda Maalum ya D’salaam ya ukamataji wa makosa ya Usalama Barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 21.08.2016 hadi tarehe 22.08.2016 ni kama ifuatavyo:-
- Idadi ya magari yaliyokamatwa 5,346
- Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa 216
- Daladala zilizokamatwa 1,121
- Magari mengine (binafsi na malori) 225
- Jumla ya Makosa yaliyokamatwa 20,562
Jumla ya fedha za Tozo zilizopatikana TSH 161,750,000/=
S.N.SIRRO – CP
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM




No comments:
Post a Comment