Wakati viongozi wa dini wakiendelea na jitihanda za kusaka suluhu kati ya upande wa Serikali na Chadema kuhusu namna ya kuzuia kwa amani kufanyika kwa Operesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA, Septemba 1, Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametoa maoni yake.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa haoni haja ya kufanyika kwa vikao hivyo vya kusaka maridhiano kwani Chadema wanachotaka kufanya kiko kikatiba.
“Sioni ni kwanini tunahangaika na vikao vya maridhiano na tahariri nyingi kuhusu shughuli ya CHADEMA kufanya operesheni yao ya UKUTA. Kuandamana ni Haki ya KIKATIBA. Tuache watu watimize Haki yao Kwa amani. Kuzuia watu kufanya jambo lao la kikatiba ndio kuvunja amani. Wanaotaka kuandamana waandamane na wanaotaka kufanya Kazi zao nyingine tuendelee na Kazi zetu. Kwanini kutekeleza Haki ya kikatiba iwe ni kuvunja amani? Kwanini?,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

No comments:
Post a Comment