Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itatoa uamuzi wa malalamiko ya washtakiwa wa mauaji ya dada wa bilionea Erasto Msuya, mnamo Septemba 27.
Mahakama ilipanga kutoa uamuzi huo jana baada ya kusikia majibu ya hoja za upande wa mashtaka.
Washtakiwa katika kesi hiyo, Miriam Stephen Mrita (41) na mfanyabiashara Revocatus Evarist Muyela (40) wanadaiwa kumuua kwa makusudi Anathe Msuya, kwa kumchinja, nyumbani kwake, Kibada Kigamboni Mei 25, 2016.
Miriam ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo alikuwa mke bilionea Msuya. Bilionea Msuya aliuawa kwa risasi Agosti, 2015 eneo la Mijohoroni, kando ya Barabara ya Arusha – Moshi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment