DENTI: Abdul Kiba Amenipa Ujauzito (Video)

TOPICS:

nasra-001Nasra akiwa ndani ya ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga, Mwenge kabla ya kuanza mahojiano.

nasra…Akiwa katika pozi tofauti.
nasra-001…Akifurahia jambo.
DAR ES SAALAM: Nasra Salum (19) ambaye ni mwanafunzi wakidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Isqama Islamic Academy iliyopo Oman, amedai kuwa msanii wa Bongo Fleva, Abdul Salehe Kiba, amempa mimba baada yakutembea naye.
Akizungumza ndani ya studio za Global TV zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam juzi, Nasra alisema alikuwa Oman alikokuwa akiishi na shangazi ndipo alipofahamiana na Abdul kupitia Mtandao wa Kijamii wa Instagram.
“Nilikutana na Abdul Kiba kupitia Mtandao wa Instagram, yeye alinitumia meseji na kuniomba namba yangu ya simu nayotumia kwenye Mtandao wa
WhatsApp, nikampa.
“Tukaanza kuchati huku akinitongoza na kunirubuni kwa maneno matamu ya kimapenzi. Nilianza kuichukia shule na
hata kugombana na shangazi yangu, sikutaka shule tena, mawazo yangu yote yalikuwa kurejea nyumbani kuonana na
mchumba wangu mpya.
“Baada ya kugombana na shangazi aliamua kunikatia tiketi kwenye ndege ya Fly Dubai na kurejea nchini kuonana na Abdul,” alisema binti huyo.
Msichana huyo ambaye wazazi wake wote ni wenyeji wa Singida, baba akiwa na asili ya Kiarabu na mama Mnyiramba, alisema baada ya kurejea nchini, alifikia
nyumbani kwa dada yake aishiye Kariakoo jijini Dar es Salaam ambako siku ya pili yake, Abdul Kiba alifika kumtembelea.
“Tangu nikiwa njiani nilikuwa nawasiliana na Abdul, baada ya kufika siku ya pili yake akaja akiwa na rafiki zake watatu, akaniomba niende nyumbani kwake Tabata, nikakubali.
“Tulipofika nyumbani kwake, muda wote nilikuwa chumbani yeye akawa anakaa sebuleni na marafiki zake wakiongea mpaka saa tisa usiku ndipo akarejea chumbani kulala. Tulilala bila kuoga na tulishiriki tendo la ndoa mara nne bila kutumia kinga (kondomu).
“Siku ya pili nilishinda pia kwake na muda wote nilibaki chumbani tu yeye akiwa na rafiki zake sebuleni. Mchana aliniletea chakula, wali kuku, usiku kama
jana yake alikuja kulala saa tisa na tulishiriki tendo la ndoa mara mbili bila kinga.”
Binti huyo alidai kesho yake alirejea kwa dada yake, akimdanganya kuwa alikuwa
Tabata kwa shangazi yake, uongo ambao ulikubalika. Tangu wakati huo, anasema kila akimpigia simu mpenzi wake huyo, hakuwa akipokea kabla ya kuamua kumblock kabisa.
“Niliamua kwenda kupima hospitali maana nilikuwa najisikia kichefuchefu, kukosa hamu ya kula na uchovu muda mwingi. Nikakutwa nina mimba, namtaka Abdul ajisalimishe, kaniharibia
maisha yangu,” alisema.
Global TV ilimtafuta Abdul na kumpa madai yote ambapo alikiri kwa kusema;
“Naomba nikuulize mwandishi, je? Wewe una miaka mingapi? (akajibiwa),
“Hivi inakuingia akilini umpe binti mimba ndani ya siku mbili igundulike? Ni kweli nilifanya mapenzi na huyo binti nyumbani kwangu siku mbili bila kinga. Lakini namuona kama anatafuta kiki kupitia jina langu siamini kama kweli ana mimba.
“Nili-mblock baada ya kuona anasumbua, kila dakika anapiga simu, si kweli kwamba anasoma, yeye aliniambia anafanya biashara Oman ndiyo maana
nilimtongoza. Achane naye.”

No comments:

Post a Comment