Diamond, Harmonize na DJ D-Ommy Washinda Tuzo Za Afrimma 2016

Staa wa Bongo Fleva Harmonize (kulia) na Dj D Ommy (kushoto) wa Clouds wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuchukua tuzo.


Tuzo za AFRIMMA ambazo hutolewa kila mwaka kwa Waafrika mbalimbali waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali hasa za burudani, zimetolewa Dallas, Texas nchini Marekani.

Wasanii wa Tanzania walioshinda tuzo ni Staa wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz, Harmonize na Dj D Ommy wa Clouds FM ambaye ameshinda Tuzo ya Dj Bora wa Afrika kupitia shoo mbalimbali ikiwemo XXL na AMPLIFAYA. Harmonize ameshinda tuzo ya msanii bora chipukizi Afrika 2016 huku Diamond Platnumz akishinda ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment