BILIONI 59.9 KUNUNUA VIFAA VYA TEZI DUME

KIASI cha Sh bilioni 59.5 kimeidhinishwa kwa ajili ya kununua vifaa tiba vya kisasa katika hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo mkoani hapa, ikiwemo mashine kwa ajili ya matibabu ya tezi dume na upasuaji wake.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Alphonce Chandeka alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juzi.

Alisema kiasi hicho cha fedha kimeidhinishwa kununua vifaa tiba vya kisasa ili Watanzania wapate huduma zinazostahili na serikali kutoingia gharama za kupelekwa wagonjwa kutibiwa.

Chandeka alisema kati ya fedha hizo zilizoidhinishwa na serikali Sh bilioni 16 zimetengwa kwa ajili ya kununua mashine za kisasa katika ukanda wa Jangwa la Sahara za MRI, CT Scan, Digital Xray na mashine nyingine za uchunguzi.

No comments:

Post a Comment