Kesi ya Mke wa Bilionea Msuya Yaahirishwa Tena

msuya-1

DAR ES SALAAM: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kutoa uamuzi wa maombi ya Miriam Msuya aliyekuwa mke wa bilionea jijini Arusha, marehemu Erasto Msuya, kuhusu kufutiwa mashitaka ya madai ya kumuua wifi yake, Anethe Msuya yaliyotokea Mei 25, mwaka huu, Kigamboni, Dar.
msuya-2Miriam Msuya akitoka mahakamani baada ya kesi kuahirishwa.
Uamuzi huo ungetolewa leo lakini kesi imeahirishwa kwa kuwa, Hakimu Mkazi Magreth Bankika anayesikiliza kesi hiyo, hakuwepo mahakamani.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa, alisema kesi ilitajwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi lakini hakimu anayeisikiliza hakuwepo hivyo uamuzi utatolewa Desemba 8, mwaka huu.
NA DENIS MTIMA/GPL

No comments:

Post a Comment