MADAKTARI BINGWA WA MOYO WATOA HUDUMA YA MATIBABU YA MOYO BILA YA KUPASUA KIFUA (CATHETERIZATION) KWA MGONJWA.

Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari wenzao  kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia wakitoa huduma ya  matibabu ya moyo bila ya kupasua kifua (Catheterization) kwa mgonjwa. Kushoto ni Afisa Muuguzi Ayoub Mchau, akifuatiwa na Dkt. Daniel Maclennan na kulia ni Dkt. Peter Kisenge.
Afisa Muuguzi wa  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Ayoub Mchau akiendelea na maandalizi ya kazi ya kutoa huduma ya  matibabu ya moyo bila ya kupasua kifua (Catheterization) kwa mgonjwa huku Dkt. Daniel Maclennan (kulia) na  Dkt. Peter Kisenge (katikati) wakimtazama. Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia hivi sasa iko katika kambi maalum ya  siku sita ya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo na katika kambi hiyo wagonjwa 20 wanarajiwa kupata matibabu.

No comments:

Post a Comment