MZAZI AZUILIWA KUONDOKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KWA KUSHINDWA KULIPA SHILINGI 338,257

Mzazi Sakina Lembo

Na Dotto Mwaibale
MZAZI Sakina Mohamed Lembo (26) pichani mkazi wa Mbagala Kibonde Maji amezuiliwa kuondoka wodi ya wazazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), kutokana na deni la sh. 338,257 baada ya kufanyiwa oparesheni ya uzazi.

Akizungumza na mwandishi wodini hapo Dar es Salaam leo, Lembo  alisema hajui hatma yake kwani yeye na ndugu zake hawana uwezo wa kulipa fedha hiyo ambayo kila siku imekuwa ikiongezeka kama riba.

Mama mzazi wa Salome, Edith Chausa akizungumza na mtandao huu alisema mwanaye alifikishwa katika hospitali hiyo Novemba 15, 2016 akitokea Hospitali ya Serikali ya Zakhem ambapo walimuandikia rufaa kwenda MNH baada ya kubaini alikuwa na dalili za kifafa cha mimba.

No comments:

Post a Comment