Wanafunzi waliohitimu na kutunukiwa Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakishangilia wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo, alitunuku jumla ya wahitimu 733. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG}
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo,akimtunuku Evelyn Wallace Shundi Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
Wahitimu Agnes Nsokolo (kulia) na Asha Kidendei wakiwa na furaha baada ya kuwa miongoni mwa wahitimu 43 waliotunukiwa Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment