Wanasayansi Udsm Wafurahia Kuhitimu

udsm-1

Wahitimu mbalimbali wa kozi za masomo ya sayansi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja.
udsm-2Wahitimu wakipiga picha nje ya Ukumbi wa Nkrumah wa chuo hicho.
udsm-3…picha zikiendelea kwa wahitimu hao.
udsm-4….picha mbalimbali za kumbukumbu zikiendelea.
udsm-5…wakipiga picha katika moja ya vibao vinavyoonyesha jina la chuo hicho.
udsm-6Mmoja wa wanandugu wa wahitimu hao (katikati) akipozi nao.
Na Denis Mtima/Gpl
WANACHUO wa kitengo cha sayansi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mapema leo wameonekana wakifurahia kuhitimu masomo yao ambapo kamera yetu imewashuhudia wakipiga picha mbalimbali chuoni hapo kabla ya kuelekea kwenye Ukumbi wa Mlimani City, kulipofanyika sherehe za mahafari ya 46 ya chuo hicho.
Mmoja wa wahitimu hao aliyejitambulisha kwa jina la Dauson Amos akizungumza na mtandao huu alisema, anamshukuru Mungu kwa kuweza kuhitimu masomo yake hayo ya sayansi.
Mbali na mahafari hayo kwa wanasayansi, mahafari mengine kwa ajili ya kozi nyingine chuoni hapo yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment