MZEE Athuman Mchambua (76), ambaye ameweka tangazo nyumbani kwake la kutafuta mke, ameongeza sharti jipya kwa mke anayemuhitaji.
Amesema licha ya kupokea simu nyingi kutoka maeneo mbalimbali nchini, lakini amewataka wanawake ambao atawafanyia usaili, hasa kwa yule ambaye atakuwa ameshinda, kutobweteka kwani atakuwa katika kipindi cha mpito cha ndoa yake.
Mzee huyo amelieleza gazeti la Mtanzania kuwa amefikia hatua hiyo ili kuanza kupitia majina ya wanawake zaidi ya 30 ambao tayari wamejaribu bahati ya kuolewa naye.
Alisema kuwa haoni haja tena ya kuendelea kuweka tangazo hilo kwa kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanaojitokeza hushindwa kukidhi vigezo anavyovihitaji.

No comments:
Post a Comment