Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez amewahamasisha vijana mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa zilizopo katika malengo endelevu ya Dunia ilikuwezeshwa kimafunzo na mitaji zaidi. Akizungumza katika semina maalum ya FURSA 2016 kwa mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na Clouds Media kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) na wadau wengine mbalimbali huku wananchi kutoka maeneo tofauti wamepata kuhudhuria, Bw. Alvaro amesema vijana na wananchi wanayo fursa ya kuchangamkia malengo hayo ya endelevu.
“Tumeweza kuzunguka maeneo mbalimbali ya Tanzania kuwafundisha vijana kuwa mabalozi wa malengo endelevu ya Dunia. Na zaidi ya vijana 10,000 kwa kufikiwa na elimu ya maendeleo endelevu. Ikiwemo Iringa, Kigoma Mbeya na mikoa mingine” amesema Bw. Alvaro. Aidha kwa upande wa washiriki wengine wakiwemo watoa mada wameweza kutoa shuhuda mbalimbali za mafanikio na namna ya kupata elimu ya kibiashara.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa elimu kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana walioshiriki kongamano la Fursa 2016 jijini Dar.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mh. Richard Kasesela akizungumza kwenye kongamano la Fursa 2016 kwa vijana liliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Mtana, Millenium Towers.
No comments:
Post a Comment