Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), kimesema kipo kwenye maandalizi ya kumkabidhi kadi mrembo wa Tanzania mwaka 2006, Wema sepetu, pamoja na kundi lake lenye zaidi ya watu 500.
Wema alikuwa mmoja kati ya wanachama maarufu wa CCM katika kundi la wasanii wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka juzi kwa kaulimbiu ya ‘mama ongea na mwanao’.
Akiwa kama kiongozi wa wasanii, alishiriki kumnadi Mgombea Mwenza wa CCM ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Katika mkutano wake na wanahabari mwishoni mwa wiki, Wema alisema kwa sasa ameamua kuvaa magwanda na yupo tayari kwa mapambano.
Mkuu wa Idara ya Habari wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Tumaini Makene jana alisema wapo kwenye maandalizi na kabla ya Machi 5, mwaka huu watamkabidhi Wema kadi ya uanachama na kundi lake linalomuunga mkono.
No comments:
Post a Comment