MKE WA BILIONEA MSUYA AACHIWA HURU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatus Muyela wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya Aneth Msuya.
Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa leo (Alhamisi) amewaachia huru washtakiwa hao baada ya upande wa mashtaka kushindwa kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ya mauaji ya kukusudia iliyokuwa ikiwakabili mahakamani hapo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya jalada la kesi hiyo lililokuwa limeitwa Mahakama Kuu kurejeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Februari 20, 2017 Hakimu Mwambapa aliupa upande wa mashtaka muda wa siku tatu kurekebisha hati ya mashtaka.

No comments:

Post a Comment