Dar/Mikoani. Mtu anapopatwa na jambo, ni kawaida ya binadamu kuangalia mambo au kauli zake alizokuwa akitoa kabla ya kufikwa na tukio hilo.
Mara nyingi mambo au kauli hizo huonyesha kama vile alikuwa akiona tukio likimjia au kumtokea.
Unaporejea kauli za hivi karibuni za Nape Nnauye, unaona dhahiri kuwa alikuwa kama anaona kinachokuja na kujitabiria kuwa angevuliwa uwaziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo.
Kauli ya mwisho na yenye nguvu aliitoa juzi mchana wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tukio la uvamizi wa studio za televisheni za kampuni ya Clouds Media Group.
“Niseme tu kwamba nimepokea ripoti na kama nilivyosema kazi hii si rahisi sana, ina gharama kubwa sana. Gharama ya kusimamia haki, kusimamia ukweli,” alisema juzi.
No comments:
Post a Comment