Rais Magufuli amtaka Makonda aendelee kuchapa kazi

Rais John Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuendelea kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwasababu yeye ndiyo Rais wa nchi hii.
Rais Magufuli amesema kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiyo mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.
Mkuu huyo wa nchi amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo badala ya kupoteza muda kufuatilia udaku kwenye mitanfandao.
"Mimi ni rais ninayejiamini, sipangiwi mambo ya kufanya. Hata fomu ya kugombea nilikwenda kuichukua peke yangu, kwa hiyo Makonda wewe chapa kazi," amesema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment