TAARIFA:
SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) linakanusha Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maji Safi na Maji taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), kuhusu kukosekana kwa Huduma ya maji kwa siku ya Jumapili tarehe 12/03/2017 kwa wakaazi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ili kupisha TANESCO kufanya matengenezo ya ukamilishaji kazi ya kuunganisha umeme kwenye mtambo mpya wa maji wa Ruvu Juu.
Aidha, Taarifa hiyo ya DAWASCO iliainisha kuwa ukosefu huo wa Huduma ya maji unatokana na matengenezo yatakayofanywa na TANESCO kwa siku husika.(12/03/2017).
TANESCO inapenda Umma ufahamu yafuatayo;
Mosi, TANESCO ilipokea ombi la DAWASA kupitia Mkandarasi wao (M/s Mollel Electrical Engineering) wiki iliyopita la kuomba kuzimwa umeme ili wakamilishe kazi ya mradi wa kuongeza mashine za kusukuma maji kwenye kituo cha Ruvu juu kilichopo Mlandizi, kupitia mradi huo mashine nne zinazohitaji megawati 2 kila moja zimefungwa
Wataalam wa TANESCO waliishauri DAWASA wajenge laini ya kilovolti 33 kutoka Chalinze hadi Mlandizi ili kuzipatia umeme mashine hizo mpya walizoongeza.
Pili, Baada ya wataalam wa TANESCO kutembelea eneo hilo na kufahamu uharaka wa mradi huo wa maji kwa Wananchi ilishauri DAWASCO kwa barua kuwa umeme uzimwe siku ya ijumaa tarehe 10/03/2017 ili Mkandarasi wa DAWASCO
No comments:
Post a Comment