Zaidi ya Wanafunzi 600 wa shule ya sekondari ya Bariadi Mkoani Simiyu wameandamana na kufunga barabara kuu ya Bariadi –Lamadi kupinga kuhamishwa kwa mkuu wa shule hiyo Deus Toga ambaye alipata uhamisho wa kwenda shule ya sekondari Giriku.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa tano asubuhi katika barabara hiyo na kusababisha kusimama kwa shughuli za mji huo ambapo lilidumu kwa muda wa masaa mawili hadi polisi walipoingilia kuwatawanya.
Wanafunzi hao walikuwa wakiandamana kutoka shuleni kwenda katika ofisi ya mkurugenzi wa mji wa bariadi, umbali wa kilomita 1, lakini ilishindikana baada ya kikosi cha jeshi la polisi cha kuzuia ghasia (FFU) kuwadhibiti wanafunzi hao.
Aidha wanafunzi hao wakiwa katikati ya barabara waliamua kugeuka na kuandamana tena kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa jambo lililoshindikana baada ya askari hao kuwazuia wakiwa wamefika eneo la Hospitali teule ya mkoa (somanda).
No comments:
Post a Comment