Sumbawanga. Mkazi wa Kijiji cha Msia wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, Patrick Kipesa (39) amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani mara baada ya kuumua mkewe kwa kumkata kata na shoka sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Polycarp Urio amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana saa 1:30 asubuhi katika Kijiji cha Msia wilayani Sumbawanga.
Alimtaja aliyeuawa kuwa ni Theresia Selemani (49) mkazi wa kijiji cha Msia aliuawa kwa kukatwa katwa na shoka maeneo ya kichwani na shingoni na mume wake huyo.
Amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa naye alijiua kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani akiwa sebuleni kwake na kufariki papo hapo.
No comments:
Post a Comment