Mfanyabiashara wa Uganda, Ivan Semwanga amefariki dunia katika Hospitali ya Steve Biko Academic jijini Pretoria, nchini Afrika Kusini.
Zari aliyezaa watoto watatu na mwanamume huyo amethibitisha kifo chake kwa kuandika katika mtandao wa Instagram akimtakia pumziko la milele.
“Mungu huwaita kwake walio wema ndiyo maana amekuchukua. Umegusa maisha na kusaidia wengi. Nakumbuka ulikuwa ukiniambia maisha mafupi acha ufurahie, sasa naelewa ulichokuwa ukimaanisha… utakumbukwa daima,” anaandika Zari ambaye alitengana na mzazi mwenzake huyo kabla ya kuwa na mahusiano na staa wa muziki hapa nchini, Diamond Platnumz aliye zaanaye watoto wawili.
Anakumbukwa kwa staili yake ya maisha ya kuonyesha fedha katika mitandao ya kijamii na kuzigawa kwa watu wenye mahitaji mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment