NYEPESI NYEPESI KUTOKA HOSPITAL YA MERCY, SIOUX CITY IOWA

Tunakumbuka watoto watatu waliojeruhiwa kwenye ajali ya basi la Wanafunzi Karatu, Arusha wako Marekani katika Hospitali ya Mercy, Sioux City Iowa kwa matibabu. Jiririshe na video hii na unaweza kugundua kuwa licha ya Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kujifanya mstari wa mbele kama ni mtu aliesaidia watoto hawa kwenda kutibiwa nje siyo habari za kweli bari ni wazungu ambao walikuwa safarini Serengeti kitalii ndiyo walifanikisha safari hii kutokana na roho yao ya kusaidia wakiwa kama madakitari wa hospitali ya Mercy. Chakusema hapa viongozi waache kujitengenezea sifa kwenye majanga ya kitaifa kama haya. Habari kamili inakuja kaa nasi Vijimambo blog kutoka U.S.A juu ya ukweli mzima wa safari ya watoto hawa. Mungu awaponye haraka kwa uwezo wake na kwa nguvu za madakitari wa Mercy, Sioux City.

No comments:

Post a Comment