Na Vero Ignatus, Arusha.
Mwanamke mmoja mkazi wa Levolosi Arusha bi Rehema Juma Kishena (40) anawaomba watanzania wenye mapenzi mema kumsaidia kupata fedha ya matibabu kutokana na tatizo la uvimbe linalomsumbua katika shavu lake la kulia ambalo limezunguka taktibani robo tatu ya uso wake . Mwanamke huyo ambae ni mama wa watoto (4) amesema kuwa tatizo hilo lilimuanza kwa jino kuumua, akachukua hatua ya kwenda hospitalini kuling’oa , mwaka 2001 uvimbe ulijitokeza katika jino alilong’olewa, na kupelekea kufanyiwa upasuaji, baada ya miaka mitatu uvimbe ulirudi tena kama awali.
‘’Jino lilikuwa linaniuma nikaenda hospitalini kuling’oa, ndipo ukaanza uvimbe kwenye jino nililongoa nikarudi hospitalini wakaniambia nifanyiwe upasuaji ili kuondoa uvimbe ,baada ya miaka mitatu tatizo hilo likajirudia kama lilivyokuwa mwanzo “alisema Bi. Rehema.
Amesema kuwa kwa sasa hana msaada wowote kwani wazazi wake ni wazee, hawana mwezo wa kumsaidia,yeye mwenyewe hana mume kwani alimkimbia wati alipoona tatizo linaendelea kuwa kubwa.
No comments:
Post a Comment