Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeanza kutekeleza operesheni iliyoitangaza wiki iliyopita kwa kuwaondoa wapigadebe kwenye vituo vya daladala kutokana na kuwa chanzo cha wizi.
Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Lucas Mkondya, jana alisema kuwa, operesheni hiyo imeanza jijini baada ya kukithiri kwa kesi zitokanazo na wizi kwenye vituo hivyo.
Alisema kwa siku kunaripotiwa matukio 20 hadi 50 ya wizi kwenye vituo vya daladala jijini huku wapigadebe wakidaiwa kuwa kichaka cha wizi huo.
Alisema operesheni hiyo, itakayoendeshwa kwa wiki nzima imelenga kuvifanya vituo hivyo kuwa maeneo salama.
“Vituoni kunakuwa na wizi na wezi wanafahamika, sasa ni mkakati wa kuwaondoa na kama wiki ikimalizika wizi haujaisha, tutawaondoa wote ambao hawana shughuli maalum vituoni hata kama hawapigi debe,” alisema.
No comments:
Post a Comment