Mchungaji Peter Msigwa.
MBUNGE wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema polisi hawawezi kumpangia nini cha kusema na wala sio majukumu yao.
“Wamenikamata nikitimiza majukumu yangu ya kibunge! Sitanyamaza,” ameandika Mchungaji Msigwa katika ukurasa wake wa Twitter.
Msigwa aliachiwa huru jana usikukwa dhamana baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Msigwa ameachiwa baada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha, Iringa Leonce Marto.
No comments:
Post a Comment