Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu amesema kwamba madaktari wa Kenya wamesema Tundu Lissu hawezi kusafirishwa kwenda nje kwa ajili ya kumpatiwa matibabu.
Mbunge Nyalandu ameeleza hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram, Facebook na Twitter kwamba mipango ya kumsafirisha Lissu ambayo walikuwa wanafanya itasimama kwa sasa kutokana na ushauri wa madaktari hao ili kuruhusu kukamilishiwa huduma za tiba ambazo tayari ameanzishiwa, hadi hapo itakavyoshauriwa vinginevyo.
Katika kurasa zake hizo za mitandao ya kijamii Nyalandu ameandika hivi, “Tunafahamu kwamba, tangu Alhamisi, Septemba 7, siku ambayo Mh #TunduLissu, Mb., (Singida Mashariki-CHADEMA) alishambuliwa kwa kupigwa risasi mjini DODOMA, Watanzania wengi wamesononeshwa na kulia sana, na kubwa zaidi, WOTE wameungana katika kuomba Sala na Dua kwa ajili ya Mh #TunduLissu, ili mkono wa Mkombozi, aliye MUNGU wetu, upate kumgusa tena na kumponya dhidi ya majeraha, maumivu na mateso anayoyapitia,”
No comments:
Post a Comment